Filamu Fupi
Jamii Salama Kwa Maendeleo

FGM Tanzania

An activist speaks to traditional leaders in Siha District, Tanzania

© Friedrich Naumann Foundation for Freedom

Filamu: Ondoa Ukeketaji – Jamii Salama kwa maendeleo.

Je, upo tayari kushuhudia mabadiliko yenye nguvu? Jiunge nasi tunapoibua hadithi za kusisimua za ujasiri, matumaini na uanaharakati katika filamu inayoangazia jinsi jamii zinavyovunja ukimya kuhusu ukeketaji. Je, viongozi wa kimila, vijana waliowezeshwa, na maghariba waliobadilishwa watafanikiwa kuunda upya mustakabali wa wasichana? Fuatilia ili kujua jinsi mradi huu wa kimapinduzi sio tu unapinga mila hatari, bali pia unachochea mabadiliko ya kudumu. Safari yako ya uelewa na utetezi inaanzia hapa!

Ukeketaji unajumuisha taratibu mbalimbali zinazohusisha uondoaji sehemu au jumla ya sehemu ya siri ya nje ya mwanamke kwa sababu zisizo za kimatibabu. Kwa jamii nyingi, ikiwemo ya kimasai, ukeketaji unaonekana kama ibada ya kupita, ambayo inaashiria mabadiliko ya msichana kuwa mwanamke. Hata hivyo, tabia hii yenye madhara huleta hatari kubwa kiafya na pia ni ukiukwaji mkubwa wa haki za wanawake na wasichana.

At this point you will find an external content that complements the content. You can display it with one click.

Wilaya ya Siha, imetajwa kuwa kitovu cha ukeketaji, ambapo kihistoria, mila na desturi za kitamaduni zimekuwa zikipuuza ustawi wa wanawake na wasichana. Mradi huu ulilenga kushughulikia ukiukwaji huu wa haki za binadamu kupitia elimu na ushirikishwaji wa jamii. Ulilenga katika kuongeza ufahamu juu ya hatari za ukeketaji na kukuza haki za binadamu huku ikiwashirikisha viongozi wa kimila na maghariba (wanawake wanaofanya ukeketaji) ili kuhimiza na kuungwa mkono kwa mabadiliko. Mradi ulitoa mafunzo kwa Gharibas 132, ambao pia walikuwa wanawandaa maghariba wengine wapya, kubadilika, kuacha ukeketaji na kuwa watetezi. Mradi uliwapa ujuzi wa ujasiriamali, na kuwawezesha kuanzisha biashara ndogo ndogo ili kuacha kutumia ukeketaji kama chanzo cha mapato. Mpango huu, ulifikia wanawake wengine 300 zaidi, ambao walikuwa na nia ya kujiunga na ughariba, na hivyo wangeongeza athari katika jamii.

Viongozi wa kimila, ambao wanaheshimiwa kama walinzi wa utamaduni, wamekuwa washirika muhimu katika harakati hii, wakitumia mamlaka yao ya kupinga ukeketaji. Vikundi vya vijana vilihamasishwa kama waelimishaji, na kuanzisha vilabu vya haki za binadamu mashuleni ambavyo vinafuatilia na kuripoti matukio ya ukeketaji, kuhakikisha kwamba sauti za vijana zinasikika katika kupigania mabadiliko. Zaidi ya hayo, msaada wa serikali umekuwa na jukumu muhimu, huku baadhi ya vijiji vikiunda sheria ndogo ndogo za kuwalinda wanawake na watoto dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.

Mpango huo umesababisha mabadiliko makubwa katika jamii. Maghariba waliokuwa sehemu ya mradi, walikubali kubadilika na kuwa watetezi, huku wakipinga kanuni za kitamaduni zinazohusisha ukeketaji. Mafanikio haya ya mradi yameleta msukumo kwa jamii jirani za Kimasai, kupinga mila hii potofu.

Mradi wa Jamii Salama kwa Maendeleo unaweza kutumika kama kielelezo cha mafanikio cha ushirikishwaji wa jamii, elimu, na uwezeshaji katika vita dhidi ya ukeketaji. Ili kushughulikia mizizi ya kitamaduni na mila ni muhimu kushirikiana na viongozi wa kimila na  kutoa njia mbadala kwa Maghariba za kujipatia kipato. Hii ni mbinu mojawapo katika kulinda afya na ustawi wa wanawake na wasichana.